break

vt,vi 1 vunja, pasua; vunjika, katika he broke the cup alivunja kikombe the rope broke kamba ilikatika it broke in two ilipasuka vipande viwili. ~ the law/one's word vunja sheria/ahadi ~ a journey vunja safari. 2 haribu. ~ a radio haribu redio his health broke afya yake iliharibika. 3 (of dog, horse etc) tia adabu, zoesha, fundisha, fuga a well broken horse farasi mwelekevu. 4 ~ the back of maliza sehemu ngumu. 5 ~ the bank filisi. 6 (mil) ~ bounds toka bila ruhusa. 7 ~ cover jitokeza (baada ya kujificha). 8 ~ even fanya biashara bila hasara wala faida. 9 ~ faith saliti. 10 ~ new/fresh ground lima sehemu mpya; (fig) anza kazi/mwelekeo mpya. 11 ~ heart vunja moyo, katisha tamaa. 12 ~ the ice anza urafiki, ondoa ubaridi. 13 ~ a man dhili, vunja, lazimisha kutoa siri. 14 ~ the news tangaza/toa habari. 15 ~ an officer fukuza afisa. 16 ~ open vunja, fungua kwa kutumia nguvu. 17 ~ short vunja. 18 ~ step -tofuata mipigo, paraganya mwendo. 19 ~ wind jamba, shuta. n 1 mpasuko; mvunjiko; mpasuo. 2 ~ of day/day ~ mapambazuko. 3. mapumziko without a ~ bila kupumzika. 4 tofauti, badiliko, usumbufu ~in one's way of life mabadiliko katika mwenendo wa maisha ya mtu. 5 nafasi, wasaa give somebody a ~ mpa mtu nafasi. 6 (colloq) bahati a lucky ~ bahati njema. 7 make a ~ (for it) toroka. breakfast n kustaftahi; kifungua kinywa, kisebeho. breakwater n ukuta wa kuvunja nguvu ya mawimbi. ~ neck speed n mwendo wa hatari. breaker n wimbi kubwa lenye povu (linaloishia mwambani au pwani). circuit ~er n (elect) kikate. breakage n 1 mvunjiko. 2 mahali/sehemu iliyovunjika. 3 (usu pl) vitu vilivyovunjika, hasara inayotokana na kuvunjika kwa vitu. breakable adj pekechu, -a kuvunjika (kwa urahisi). ~ away vi 1 (prisoner) toroka. 2 (politics) jitoa, jitenga. 3 (habits) acha. ~ down vt,vi 1 vunja, bomoa, haribu; haribika, my car has broken down gari langu limeharibika peace talks have broken down mazungumzo ya amani yamevunjika. 2 (of person) vurugikiwa, changanyikiwa. 3 ainisha ~ down expenditure ainisha matumizi. 4 meng'enyuka, sababisha mabadiliko ya kikemikali. n 1 kuharibika. 2 uainishaji takwimu. 3 nervous ~down n kurukwa na akili. broken down adj -liokwisha. ~ in vt 1 ingia jengo kwa nguvu. 2 ~ (on, upon) (interrupt) ingilia. 3 funza, tia adabu n wizi ndani ya nyumba. ~ into vt 1 see ~ in 2 anza (ghafla) he broke into a run/song alianza kukimbia/kuimba. 3 tumia sehemu ~ into one's savings tumia sehemu ya pesa zilizohifadhiwa. ~ off vt vi 1 acha kusema, katiza maneno. 2 pumzika. 3 vunja. ~ off relations vunja uhusiano. 4 (of food) mega. ~ out vi 1 tokea ghafla. 2 toroka. n kutoroka. ~ through vt,vi 1 penya, tengua. 2 shinda. 3 songa mbele (licha ya upinzani). n 1 kupenya. 2 mwelekeo mpya. 3 (of discovery) uvumbuzi. 4 mafanikio mapya. ~ up vt,vi 1 vunja; vunjika. 2 (of persons) fifia. 3 (of school) anza likizo. 4 (of work) gawanya. 5 (of gatherings) tawanya. 6 (of marriage) tengana. 7 (US) chekesha sana n kuvunjika; mgao.