book

n 1 kitabu read a ~ soma kitabu. chequebook n kitabu cha cheki/hundi exercise ~ daftari go by the ~ shikilia mno sheria. 2 the B~ n Biblia swear on the B~ apa, kula kiapo. 3 kitabu, bunda (la tiketi, stempu n.k). bring to ~ toa hesabu; shtaki; patisha adhabu kwa kosa bring somebody to ~ adhibu; -taka ajieleze vitendo vyake. 4 (pl) hesabu, kumbukumbu za biashara. keep the ~s weka hesabu. be in somebody's good/black/bad ~s pendeza/topendeza mtu fulani take somebody's name off the ~s futa jina lake katika orodha ya wanachama read a person like a ~ tambua vema nia ya mtu speak by the ~ -wa na tarifa sahihi speak without ~ eleza habari kutokana na kumbukumbu take a leaf out of a person's ~ iga (matendo ya) mtu fulani that suits my ~ inanifaa. 5 ~ case n kabati ya vitabu, kasha la vitabu. book-keeping n uwekaji hesabu. bookkeeper n. book-maker n 1 mtengeneza vitabu. 2 mpokeaji fedha za bahati nasibu/dau/mashindano ya farasi. ~ marker n kalamu, kifaa cha kuwekea alama katika kitabu.~ -seller n mwuza vitabu. ~-shop n duka la vitabu. ~-stall n genge au kibanda cha kuuzia vitabu, magazeti (n.k.). ~ stand n see ~ stall. ~-store n (US) duka la vitabu. book-worm n 1 siridado. 2 (fig) mpenzi wa vitabu, msomaji sana, mbukuzi. vt 1 andika katika kitabu. 2 (of the police, traffic wardens) fungua mashtaka ~ somebody for loitering fungulia mashtaka kwa kuzurura. 3 weka /shika nafasi (kwa ajili ya safari, michezo n.k.), weka nafasi, (of hotel) chumba ~ through to kata tiketi ya moja kwa moja. fully ~ed up imejaa. ~ing office n ofisi ya tiketi. bookable adj -a kushikika, a kununulika. booking n mpango wa kushika/kuweka nafasi (ya safari, mchezo n.k.) adj -a kuagiza (au kuagizwa kutoa) tiketi. ~ing-clerk n karani auzaye tiketi (za safari). ~ binding n ujalidi; kujalidi vitabu. ~ binder n. ~-end n (pl) kishikiza vitabu. bookish adj 1 -a kuhusu vitabu, (of person) -a kupenda kusoma vitabu, -a kujua maarifa ya vitabuni tu. 2 (of style) mtindo wa lugha ya vitabuni. bookplate n utepe wenye jina la mwenye kitabu. ~-post n upelekaji vitabu kwa posta (kwa gharama ndogo). ~-rest n kitegemezi cha vitabu mezani. bookie n (sl) see book-maker.