block
n 1 pande kubwa (la mti, jiwe, n.k.). 2 bloku: jengo kubwa lenye fleti, ofisi, maduka n.k. 3 kizuizi traffic ~ /jam n msongamano wa magari barabarani. road ~ n kizuizi cha barabarani. 4 eneo lililo kati ya barabara nne zinazokutana. 5 vipande vya matofali ya saruji au mawe vya kujengea. 6 (pulley) kapi, gofia, roda. 7 kibao (kipande cha mti au chuma chenye herufi/sanamu zilizochorwa juu ya kipande hicho zikiwa alama ya chapa. 8 sehemu kuu ya injini ya petroli yenye silinda na vali. have a ~ against something pata kizuizi katika kufanya jambo. 9 mgawanyo wa viti katika jengo la maonyesho ya tamthilia, sinema n.k. 10 kichwa (k.m. kichwa cha mtu) I'll knock your ~ off nitakukata kichwa chako. 11 kiolezo cha kofia zinapotengenezwa. vt ~ (up) zuia, ziba. ~ in chora umbo, mpango wa sanamu au ramani bila kuchora kila kitu; funga. ~-chain n mnyororo (wa baiskeli). blockade n 1 uzio wa kuzunguka jeshi; zingio run a ~ade epuka/penya. 2 (US) zuio, kizuizi. vt 1 husuru, zunguka kwa vita 2. zingia, zingira na zuia (mji au ngome). blockage n 1 hali ya kuzuia. 2 kikwazo. ~ head n (colloq) mjinga, kichwangumu, baradhuli. ~ house n ngome yenye matundu ya kupenyeza bunduki. ~-letters n herufi kubwa zilizotengwa.