bleed

vt,vi 1 (draw blood) toa damu,tokwa na damu. ~ freely tokwa na damu chapa. 2 (extort) toza fedha mno. ~ someone white chukua fedha zote za mtu. 3 ~ for onea imani/huruma my heart ~s for him namwonea huruma sana. 4 (of plant) toa utomvu. 5 (of dye) chururika, churuzika. 6 (of air, water, gas etc.) toa upepo, maji, gesi n.k. kutoka katika chombo. bleeding n (of plants) machozi ya mti, utomvu. bleeder n 1 mtu mwenye mhina (ugonjwa wa kutokwa damu). 2 (sl) mshenzi. 3 (sl) jamaa. ~ing-heart n 1 mtu mwenye huruma nyingi mno. 2 aina ya mimea (hasa bustanini) yenye maua yaliyo na umbo la moyo.