barge

barge

1 n 1 tishali: mashua kubwa ya bapa itumiwayo kupakulia na kupakilia mizigo (na watu) bandarini, mitoni na kwenye mifereji. ~ man n mwendesha tishali. 2 mashua ya meli ya vita itumiwayo na maofisa. 3 mashua kubwa ya makasia itumiwayo kwa shughuli za sherehe.~ pole n upondo. (colloq) I wouldn't touch him with a ~ pole namchukia sana au simwamini kabisa.

barge

2 vi,vt 1 (colloq) gonga, gongana, ingia ghafla na kwa vishindo he ~ed into a wall aligonga ukuta they ~ed into each other waligongana he ~ed in on them while they were in a meeting aliwaingilia ghafla mkutanoni. 2 (about) enda kwa haraka na ovyo ovyo. 3 ingilia he ~ed into our discussion aliingilia mazungumzo yetu.