back

back

1 n 1 (of human body) nyuma; mgongo: sehemu ya mwili kuanzia shingoni hadi mwisho wa uti wa mgongo. backbone n uti wa mgongo. ~ ache n maumivu ya mgongo. ~ to front mbele nyuma. talk behind someone's ~ sengenya. lie on one's ~ lala chali. break one's ~ vunja uti wa mgongo, (fig) menyeka (na kazi). break the ~ of maliza sehemu kubwa/ngumu ya kazi. get off someone's ~ acha kumsumbua. put one's ~ into zamia/fanya kwa nguvu zote. turn one's ~ on kana, kwepa. with one's ~ to the wall kabiliwa na hali ngumu, zongwa na maadui. 2 egemea. have/get one's own ~ (on somebody) (colloq) jibu mapigo, lipiza kisasi. 3 sehemu ya kitu isiyotumika sana au kuonekana kwa urahisi. 4 (sport) beki.

back

2 adv 1 nyuma. go ~ (up) on/ from one's word vunja ahadi ~ and forth nenda rudi, huku na huko, mbele na nyuma. 2 (place/condition) -pa awali put ~the book rudisha kitabu mahali pa awali. 3 jibu, rudishia If I hit you, would you hit me ~? kama nikikupiga utanirudishia. 4 zamani, zama za zama, -liopita.

back

3 vt,vi 1 rudi(sha) nyuma. ~ the oars; ~ the water rudisha chombo nyuma kwa kasia. 2 ~ (up) unga mkono. 3 wekea dau. 4 ~ down (from) ghairi. ~ out of jitoa. 5 bambia, funika. backer n mweka dau; mfadhili. backing n msaada; wafadhili; ala; waitikiaji. backache n see back1. backbencher n mbunge (asiye na cheo kingine bungeni). backbite vt,vi sengenya, teta. backbiter n. backboard n 1 mwegamo. 2 kiegemeo. backbone n 1 see back1. 2 (fig) nguzo, tegemeo. 3 (reliability) utumainifu; uhodari he has no ~ yu dhaifu, yu legelege (wa tabia). backbreaking adj (of work) -a sulubu. backchat n ufyosi, majibu ya karaha/kijeuri. ~ date vt weka tarehe ya nyuma. backdoor n mlango wa nyuma. ~ drop n pazia la nyuma (la jukwaa lililorembwa kuonyesha mandhari). backfire 1 vi lipuka (mapema) ndani ya injini. 2 (fig) enda kinyume cha matarajio, enda upogo n mlipuko katika eksozi. background n 1 usuli. 2 mahali pa nyuma (sehemu ya sanamu, picha n.k.). 3 mahali pa kufichia. 4 muziki wa chinichini. backhand n kitengelenyuma. backhanded adj a (kutumia) kitengelenyuma. ~ hander n 1 kofi la kitengelenyuma. 2 rushwa. backlash n 1 uduto wa gurudumu. 2 upinzani (hasa dhidi ya siasa au sera iliyoonekana kuungwa mkono awali). backlog n kiporo, limbikizo: kazi ambayo haikumalizika. ~ number n toleo la nyuma (la gazeti); kitu (chochote) cha zamani; mtu mwenye mawazo ya kizamani. ~pay n karisaji: malipo ya (fedha ya) nyuma. ~ seat n kiti cha nyuma cha gari. take a~ jiweka nyuma nyuma. backside n (colloq) makalio, matako. backslide vi 1 rudia mazoea mabaya. 2 kengeua. backspace n (of typewriter) kurudisha nyuma. backstage n nyuma ya jukwaa (la sanaa za maonyesho). (pl) ngazi ya nyuma. backstays n (naut) (pl) kamba za kikono cha mlingoti (zinazoelekea tezi). ~ street n uchochoro; (pl) mitaani. ~ stroke n 1 pigo la nyuma. 2 mtindo wa kuogelea kimangalimangali/kichali. ~ sword n upanga. ~ track vi 1 rudi ulikotoka. 2 badilisha/legeza msimamo. backwash n mkondo wa maji.