at

prep 1 (indicating place) -ni, kwa ~ home nyumbani ~ someone's kwa fulani. at-home n tafrija inayofanyika nyumbani kwa wakati uliopangwa. 2 (indicating direction or goal) aim ~ lenga throw ~ rushia. 3 (indicating action) ~work kazini the children are ~ play watoto wanacheza she is good ~ athletics yeye ni hodari katika riadha. 4 (indicating time) ~ once mara moja ~ five saa kumi na moja ~ first mwanzoni ~ last hatimaye, mwishoni. 5 (value) bei ~ two shillings a kilo shilingi mbili kwa kilo ~ a loss kwa hasara. 6 ~ war vitani ~ rest mapumzikoni ~ length kwa kirefu; (Idiom) not ~ all sivyo kabisa; si kitu ~ any rate kwa vyovyote.