arm

arm

1 n 1 mkono. an infant in ~s mtoto mchanga. keep somebody at ~'s length epukana na, epuka urafiki au kuzoeana na. with open ~s kwa mikono miwili. 2 chochote kitokacho kama mkono k.m ~ of the sea mkono wa bahari, ghuba. 3 tawi kubwa (la mti). 4 sehemu ya vazi inayofunika mkono. 5 armchair n kiti cha mikono adj (fig) -a kinadharia ~ chair critic n mhakiki wa kinadharia. 6 armpit kwapa. 7 the (long) ~ of the law mamlaka ya sheria. 8 ~ hole n mkono wa vazi. 9 armlet n 1 kikuku. 2 kitambaa kinachovaliwa mkononi juu karibu na bega (hasa wakati wa msiba au kuonyesha cheo).

arm

2 n 1 (usu pl) silaha, zana za vita. in ~s -enye silaha. lay down ~s salimu amri. take up ~s jiandaa- kupigana. 2 up in ~s (about) pinga n sana na kuwa tayari kupigana. 3 arms ngao ya heshima. 4 coat of ~s n nembo. 5 tawi la jeshi, k.m. the air ~ jeshi la anga. armorial adj -a nembo, -a shajara ~ orial bearings n nembo; shajara. armada n armada: kundi kubwa la manowari. ~ment n (usu pl) 1 zana za vita (hasa mizinga ya manowari). 2 jeshi lenye silaha. 3 matayarisho ya vita. ~s-race n mashindano ya silaha. armour (U.S. ~or) n 1 vazi la kujihami wakati wa mapigano. 2 ngao chombo: bamba la metali liwekwalo kwenye chombo ili kukihami kisitobolewe na risasi au mizinga ya adui. 3 vyombo vya kivita (magari, vifaru, manowari, n.k.) vilivyowekewa mabamba ya chuma adj -enye vazi la kivita la chuma, -enye dereya. ~our plate n dereya, bamba la chuma. armourer n mtengeneza silaha; mtunzaji silaha za jeshi. armoury n 1 ghala ya silaha. 2 (US) kiwanda cha silaha. army n 1 jeshi. 2 jumuiya ya watu wenye madhumuni maalum. The Salvation ~y Jeshi la Wokovu. 3 kundi kubwa an ~y of helpers kundi la wasaidizi an ~y of red ants kundi la siafu.

arm

3 vi,vt pa silaha, pa kitu cha kulinda, tega bomu ~ with answers to likely questions tayarisha majibu ya maswali yanayoelekea kuulizwa. armed adj -enye silaha ~ed robbery unyang'anyi wa kutumia silaha ~ed forces majeshi.